THIS BLOG IS SPONSORED BY KESOM FREIGHT INTERNATIONAL | AND DOLLYWOOD
Sunday, September 2, 2007
Mwandishi: haki Tarehe: Sunday, September 02, 2007 | kiungo mahususi
Mratibu Miss Tanzania amtemtea Miss Tanzania Mpya ,
asema ni Mtanzania...

MRATIBU wa shindano la Vodacom Miss Tanzania, Hashim Lundenga amesema haoni tatizo kwa Richa Adhia kuwa Miss Tanzania licha ya kuwa mwenye asili ya kihindi.

Akizungumza Lundenga alisema kuwa mashindano ya Miss Tanzania, hayana mipaka kwa watu ambao ni Watanzania halisia na kwamba wote wana nafasi sawa kushiriki.

"Unajua kila kitu kizuri kitakuwa na kukosolewa, kila kitu kizuri hakikosi lawama, sasa sisi tunasema kama Kamati ya Miss Tanzania, msichana yeyote mwenye sifa na ni Mtanzania hata awe mzungu, madam ni Mtanzania ana nafasi ya kushiriki," alisema Lundenga.

Wakati huo huo, warembo 26 walioshiriki shindano la kumsaka Vodacom Miss Tanzania lililofanyika juzi usiku kwenye Viwanja vya Leaders Dar es Salaam, wameagwa jana katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Beachcomber, Kunduchi nje kidogo ya Dar es Salaam.

Lundenga alisema jana kuwa warembo hao walikabidhiwa vitita vyao jana jioni na kuagwa na leo watakuwa wakielekea majumbani mwao.

Katika shindano hilo lililofanyika kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni, Richa Adhia alitwaa taji na kuondoka na gari la sh 45mil, sh8mil na vidani na hereni vyenye thamani ya sh4m pamoja na tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika shindano la utembo la dunia.

Nafasi ya pili ilitwaliwa na Lilian Abel pia kutoka Kinondoni na kuondoka na sh5.5m wakati Queen David kutoka Temeke alishika nafasi ya tatu na kuzoa sh3.5m.

Mbali na warembo hao, walioshiriki ni pamoja na
Baby Lema,
Monica John (Temeke),
Latifa Warioba,
Immaculate Ngereza,
Neema Khatib,
Seprice Joseph (Ilala),
Fatma Kissoky,
Sophia Mwanyika,
Saada Hashim (Mashariki),
Khadija Sula, Prisca Emmanuel na Helga Gabriel (Ziwa).

Wengine ni Perpetua George
Gladness Katega

(Vyuo Vya Elimu ya Juu),
Cecilia Charles,
Wahyda Sylivester,
Neema Chande

(Nyanda za Juu Kusini),
Elizabeth Mahona,
Annastazia Ganja,
Marietha Richard (Kati) na Victoria Martin,
Irene Shirima,
Eva Mbando kutoka Kanda ya Kaskazini.

Mchuano wa mwaka huu ambao umepambwa na wasanii mbalimbali akiwemo Felix Wazekwa kutoka DRC Congo, THT na vikundi vingine, umedhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Redds, TanzaniteOne, Planetel, Cocacola na Community Airlines.