
Watoto X-Mass Show na Machozi Band
|
Mwandishi: haki Tarehe: Saturday, December 19, 2009 | kiungo mahususi
Rais Jakaya Kikwete Awatunuku kamisheni Maafisa wapya wa jeshi Monduli Mwandishi: haki Tarehe: Saturday, December 19, 2009 | kiungo mahususi
Majeneza yakiwa na miili ya watu saba wa familia moja waliokufa kwa ajali,Same ikiwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Kimangaro Mamba wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika leo(Jumamosi).Picha Na Hellen Mlacky Mwandishi: haki Tarehe: Saturday, December 19, 2009 | kiungo mahususi
Dr Sayoki Mfinanga..Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Dr Sayoki G.Mfinanga(Kushoto)mkurugenzi wa Muhimbili Madical Reseach Center wakati alipofungua jengo jipya la National Institute for Medical Research (NIMR)hivi karibuni lililopo Ocean Road,kulia ni Prof. David Mwakyusa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mwandishi: haki Tarehe: Saturday, December 19, 2009 | kiungo mahususi
Traffic Light Party ya Frank Mgoyo Funika Bovu.. ![]() Muaandaaji wa Traffic Light Party Usiku wa kuamkia leo Frank Mgoyo(Kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na Warembo Nuru akiwa na Bella.Nuru,Mange Kimambi Mwandishi: haki Tarehe: Saturday, December 19, 2009 | kiungo mahususi
Malighafi...Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa(NDC)Chrisant Mzindakaya(Kushoto) akiangalia moja ya malighafi ya kuzalisha chuma katika Eneo la Liganga mkoani Iringa.. Kulia ni Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar ambaye ni mjumbe wa bodi hiyo Dk Gharib Bilal na katikati ni Katibu Tarafa wa Ludewa Hivi Karibuni. Mwandishi: haki Tarehe: Saturday, December 19, 2009 | kiungo mahususi
Tshalla Muana Nae Afunika Jijini.. Mwandishi: haki Tarehe: Saturday, December 19, 2009 | kiungo mahususi
JB Mpiana Apagawisha Mashabiki Bongo... Jb Mpiana akiimba mbele ya wageni waalikwa na wanachama wa Club E Usiku wa Kuamkia Leo jijini Dar es Salaam ndani ya Ukumbi wa Ubungo Plaza Kundi zima la JB Mpiana likishambulia Jukwaaa Usiku wa Kuamkia Leo Jijini Dar es Salaam![]() Wadau MbaliMbali wakiyarudi Mangoma Usiku wa Kuamkia leo kwenye Show la nguvu la JB Mpiana jijini Dar es Salaam.Picha na Mdau Ahmed MichuziMwandishi: haki Tarehe: Saturday, December 19, 2009 | kiungo mahususi
Kuwafariji Waliokubwa na Maafa Same .... Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia jana wananchi wa Kijiji cha Mamba Miamba wilayani Same wakati wa ziara maalumu ya kuwafariji kufuatia mvua kubwa iliyoleta maafa na kuharibika kwa mali.Picha na Freddy Maro/Ikulu Mwandishi: haki Tarehe: Saturday, December 19, 2009 | kiungo mahususi
Kimwana Kutoka Rwanda Cythia Akazuba Awa Miss East Africa 2009 Mwandishi: haki Tarehe: Saturday, December 19, 2009 | kiungo mahususi
Makamu wa Rais Dr Shein akihutubia Mkutano wa Kimataifa wa Tabia Nchi huko Copenhagen juzi usiku.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais Mwandishi: haki Tarehe: Saturday, December 19, 2009 | kiungo mahususi
Yatima Group of Mbagala..THE First Lady, Mama Salma Kikwete and the Executive Director of Tanzania Portland Cement, Mr Pascal Lesoinne, present an assortment of gifts and foodstuff to children of two orphanage groups Yatima Group of Mbagala and Mother Theresa of Mburahati as Christmas gifts.The items worth 20m/-were donated by Portland Cement. Photo by John Lukuwi,MAELEZO Mwandishi: haki Tarehe: Saturday, December 19, 2009 | kiungo mahususi
Mama Tunu Pinda akikabidhiwa zawadi ya maua na mshindi wa kwanza katika shindano la Kisura wa Tanzania 2009 Diana Ibrahim.washiriki wenzake waliofanikiwa kuingia tano bora. Diana Ibrahim Ndie Kisura wa Tanzania 2009 Mama Tunu Pinda (ambaye amechaguliwa kuwa mlezi wa kituo cha kulea watoto yatima cha mkoani Rukwa) akipokea hundi yenye thamani ya shilingi milioni mbili kutoka Kampuni ya bia Serengeti aliyopewa na Meneja uhusiano wa kampuni ya bia Serengeti, Teddy Mapunda,katikati ni Jaji mark Bomani mwenyekiti wa kampuni ya bia Serengeti akishuhudia tukio hilo.Fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya kituo cha yatima kilichopo mkoani Rukwa na pia wamepewa mtaji wa kreti 20 za vita malta (kinywaji kisicho na kilevi) pamoja na cooler kama mtaji wa kuanzia kwa ajili ya kusaidia kuendesha kituo hicho. Mwandishi: haki Tarehe: Saturday, December 19, 2009 | kiungo mahususi
Ajali ya Mohamed Trans Laua Sita wa Familia Moja.. Basi la Kampuni ya Mohamed Trans lenye namba T810 AQM lililopasuka tairi la mbele na kuliparamia gari dogo aina la Asia Combi lenye namba T845 BCB lililokuwa limebeba ndugu wakienda katika sherehe ya harusi Mamba Kotela wilayani Moshi Vijijini,likiwa katika eneo la ajali jana katika Kijiji cha Kandoto wilayani Same mkoani Kilimanjaro. Ajali hiyo ya juzi ilisabababisha vifo vya watu 19 na majeruhi wengine 42.Picha na Hellen Mlacky------- Imeandikwa na Na Hellen Mlacky WATU sita wa familia moja ni miongoni mwa watu 19 waliokufa katika ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Mohamed Trans lililogongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Asia Combi katika Kijiji cha Kandoto, nje kidogo ya mji wa Same mkoani Kilimanjaro juzi. Ndugu hao ambao wanatarajiwa kuzikwa leo katika Kijiji cha Mamba Kotela, Moshi Vijijini, walikuwa wakienda katika harusi ya Egbert Maleko iliyotarajiwa kufanyika leo kijijini humo.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea..>>>>>>>> Mwandishi: haki Tarehe: Saturday, December 19, 2009 | kiungo mahususi
Rais Kikwete Azindua Jengo la NIMR...
Thursday, December 17, 2009
Mwandishi: haki Tarehe: Thursday, December 17, 2009 | kiungo mahususi
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Innocent Mungy akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma,Betty Mkwasa,Tuzo ya Mwanamke mwenye mafanikio ambayo Tume hiyo ilidhamini katika kipengele cha habari na mawasiliano kwenye utoaji wa Tuzo za wanawake zilizofanyika Dar es Salaam hivi karibuni.Wanawake 13 walipata tuzo hizo zilizoanzishwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania. Mwandishi: haki Tarehe: Thursday, December 17, 2009 | kiungo mahususi
Bash la Mkesha wa Mwaka
Mpya Canton Ohio-USA Tired of bringing in the new year in the same way every year?Make this year a year to remember! The Tanzania Associan of Canton presents, a New Year bash at Lollies Banquet hall of Belden Village. $5.00 cover charge at the door. Food, drinks, and fun! Music by DJ Kvelli of Columbus. Rap, Hip-Hop, and much more! Call 330-418-6401 or 330-575-7148 for V.I.P and info. Lolli's Restaurant and Banquet Center 4801 Dressler Road NW. Canton, Ohio 44718 Call: 330.492.6846 Toll Free: 1.877.GOLOLLI (1.877.465.6554) Fax: 330.492.0836 lollisrestaurant@aol.com Mwandishi: haki Tarehe: Thursday, December 17, 2009 | kiungo mahususi
Anna Abdallah Atunukiwa Tunzo. Mbunge viti Maalumu,Mheshimiwa Anna Abdallah akionesha fimbo ya kutembelea ikiwa ni ishara ya kusaidia watu wa Afrika Kusini waliokimbilia nchini kwao na kuwapatia ardhi ya makazi na kilimo Mkoani Morogoro mwaka 1976 alipokuwa Mkuu wa M koa huo.Sambamba na fimbo hiyoMheshimiwa Anna Abdallah alipewa Tuzo na Rais wa Afrika Kusini kutokana na mchango wake kwa watu wa nchi hiyo.Picha na Yusuf BadiMwandishi: haki Tarehe: Thursday, December 17, 2009 | kiungo mahususi
Deogratius Kakoko Balozi wa NMB katika chuo cha usimamizi wa Fedha IFM akibonyeza kompyuta ili kumpata mshindi wa bahati nasibu kwa wateja iliyochezeshwa leo kwenye makao makuu ya benki hiyo jengo la Bank House kushoto ni Meneja huduma za wateja binafsi wa benki hiyo Abdulmagid Nsekela(Kulia)Mkaguzi wa Michezo ya kubahatisha Bakar Maggid Kati ni Afisa wa Selcom Gaming. Mwandishi: haki Tarehe: Thursday, December 17, 2009 | kiungo mahususi
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa saba wa Sekta ya Utamaduni,uliopangwa kufanyika kwa siku tano,kuanzia Desemba 14,mwaka huu ,Chuo cha VETA mjini hapa wakisikiliza mada mbalimbali ikiwemo ya Utamaduni Kichocheo cha Amani iliyowasilishwa na Rose Sayore ( hayupo pichani)wa Mfuko wa Utamaduni. Picha na John Nditi Mwandishi: haki Tarehe: Thursday, December 17, 2009 | kiungo mahususi
Huu Mpango wa Kilimo Kwanza ni Wimbo tu-Askofu Pengo ------ Na Minael Msuya ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam,Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema kuna kila dalili za kukwama kwa Mkakati wa Kilimo Kwanza, kutokana na kushindwa kuelekeza nguvu za kutoa elimu kwa wakulima ili waendeleze sekta hiyo.Kwa habari Zaidi Bofya na Endelea..>>>>>>>> Mwandishi: haki Tarehe: Thursday, December 17, 2009 | kiungo mahususi
Dr Lawrence Gama Afariki Dunia MBUNGE wa zamani wa Songea Vijijini Dk Lawrence Gama(Pichani),amefariki dunia jana mchana katika hospitali ya Agha Khan baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kansa ya mapafu.Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM,John Chiligati, alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuongeza kuwa taarifa zaidi ya kifo hicho zitatolewa leo. Alisema CCM imepokea kwa mshtuko taarifa za kifo hicho kwa kuwa kiongozi huyo alikuwa ni mmoja wa wazee waliotumikia Tanzania kwa uadilifu na mfano wa kuigwa na vijana.“CCM tumempoteza mtu muhimu ambaye alijitolea kwa muda mrefu kutumikia nchi yake kwa kuwa alishika nyadhifa mbalimbali muhimu hali ambayo vijana wa sasa wanapaswa kuiiga,” alisema Chiligati. Alisema Gama katika uhai wake pamoja na kuwa mbunge ni mmoja wa waanzilishi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi(JWTZ),aliwahi kuwa Katibu wa CCM na pia aliwahi kuwa mkuu wa Usalama wa taifa nchini. Mwandishi: haki Tarehe: Thursday, December 17, 2009 | kiungo mahususi
na Warembo wa Miss East Africa Ikulu... Mshiriki kutoka Tanzania Victoria Patrick kushoto akizungumza warembo na wenzake wakatika walipokuwa Ikulu jana kwa mwaliko wa Rais Jakaya Kikwete. Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, December 16, 2009 | kiungo mahususi
Mwanamuziki kutoka Demokrasia ya Kongo Tshalla Muana akiongozana na Meneja Msaidizi chapa ya Embassy Eliza kilimbai Ndosi (shoto),mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam leo jioni kwa ajili ya onesho la Embassy Club E litakalofanyika ndani ya Ubungo Plaza ijumaa jijini Dar es SalaamMwandishi: haki Tarehe: Wednesday, December 16, 2009 | kiungo mahususi
Waanza Kulamba Asali..Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Rais Jakaya Kikwete(wa pili kulia)akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa CUF,Maalim Seif Shariff Hamad(wa tatu kulia)na Mwenyekiti wa chama hicho,Prof Ibrahim Lipumba wakati wa gwaride la kuadhimisha miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika kwenye Uwanja wa Uhuru,Dar es Salaam Hivi karibuni.Kulia ni Makamu wa Rais, Dkt.Ali Mohamed Shein.Viongozi hao ambao hivi karibuni walimtambua rasmi Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar waliitwa na kukaa kwenye jukwaa rasmi la viongozi uwanjani hapo.Picha na Emmanuel Kwitema Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, December 16, 2009 | kiungo mahususi
? Picha Moja Maneno Elfu Moja.Pichani ni Mbunge wa Urambo na Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samwel Sitta(Kushoto)Akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Fredrick Sumaye kwenye moja ya vikao vya Chama Siku za Nyuma.Mdau Tunga Kichwa cha Habari cha Picha hii. Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, December 16, 2009 | kiungo mahususi
Sauti za Busara Music Festival 2010 Yanukia... ![]() ![]() Busara Promotions PO Box 3635, Zanzibar,Tanzania +255 24 223 2423 +255 784 925 499 +255 773 822 294 Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, December 16, 2009 | kiungo mahususi
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wapya wa Tanzania katika nchi za nje mara tu baada ya kuwaapisha rasmi ikulu jijini Dar es Salaam,kutoka kushoto ni Balozi Dr.James Nzagi anayekwenda Burundi,Rais Kikwete,Balozi Bibi Salome Sijaona anayekwenda Japan na Balozi Prof.Abillah Omar anayekwenda Saud Arabia. Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, December 16, 2009 | kiungo mahususi
Mwenyekiti wa kamati ya Miss East Africa na mkurugenzi wa Rena Event Bw.Rena Calist akizungumza na wanahabari kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach and Resort leo wakati alipotangaza zawadi kwa washindi wa shindano hilo leo linalotarajiwa kufanyika Ijumaa Disemba 18 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.Picha na Mdau John Bukuku Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, December 16, 2009 | kiungo mahususi
Mkuu wa Mauzo wa Zantel Bw.John Mbaga(kulia)akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya kampuni hiyo leo wakati wa uzinduzi wa ofa mpya ya“MZUKA” ambayo itamuwezesha mteja wa Zantel kuongea kwa masaa 12 kwa Tsh 200 tu kuanzia saa nne na nusu usiku hadi saa nne na nusu asubuhi.Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Bw. Fintan Lawler. Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, December 16, 2009 | kiungo mahususi
Rais Kikwete ana Mamlaka kisheria kuwabana Mafisadi-Prof Shivji ----- Na Sadick Mtulya SIKU moja baada ya Waziri wa Sheria na Katiba Mathias Chikawe kusema Rais Jakaya Kikwete hawezi kutumia mamlaka yake kuwabana mafisadi,baadhi ya wanasheria nchini,akiwamo Profesa Issa Shivji,wamepinga kauli hiyo kwa kusema sio kweli.kwa Habari zaidi bofya na Endelea..>>>>>> Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, December 16, 2009 | kiungo mahususi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akiushika waya wa Umeme unaotokea Tanga uliopita chini ya bahari na kupandishwa jana,katika ufukwe wa Mkumbuu kisiwani Pemba,kazi hiyo inafanya kwa kutumia Meli maalum ya kampuni ya Nexans Skagerrak ya Norway. Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, December 16, 2009 | kiungo mahususi
Emelda wa Bang Magazine na Baraka Wafanya Kweli.. ![]() ![]() Kama kawaida blog hii ya Food For Thought Inapenda kumpa pongezi la nguvu Emelda wa Bang Magazine na Mumewe Baraka kwa kutimiza ahadi yao kwa Mungu na kufunga pingu za Maisha Tarehe 13/12/2009 nakufwatiwa na Sherehe la Nguvu jijini.Picha na Mdau Bernard RwebangiraMwandishi: haki Tarehe: Wednesday, December 16, 2009 | kiungo mahususi
Warembo kumi watakaoingia katika shindano la kumsaka KISURA WA TANZANIA 2009 wakionyeshwa mbele ya waandishi wa habari jijini hivi karibuni na Uongozi wa Beautiful Tanzania Agency ambao ndio wameandaa shindano hilo litakalofanyika Dec 17,2009 katika hotel ya Movenpick na mshindi atapewa shilimgi milioni tano(5m/-) Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, December 16, 2009 | kiungo mahususi
Hongera Advocate Hafsa Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Agustino Ramadhani Akimkabidhi Certificate ya Uanasheria kwa Bi Hafsa Said kwenye sherehe zilizofanyika jijini Dar es Salaam Jana.Picha na Mdau Yusuf Badi Mwandishi: haki Tarehe: Tuesday, December 15, 2009 | kiungo mahususi
Makamu wa Rais Dr Ali Mohamed Shein Akiwasili Muda Mfupi Copenhagen Denmark kushiriki kwenye mkutano wwa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.Makamu wa Rais Amefwatana na Ujumbe wa Tanzania unaojumuisha mke wake,Mama Mwanamwema Shein,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais(Mazingira)Dk Batilda Burian na Waziri wa Kilimo,Mifugo na Mazingira wa Zanzibar,Bruhani Haji Saadat. Mwandishi: haki Tarehe: Tuesday, December 15, 2009 | kiungo mahususi
DJ YOUNG KIM MAGOMERO AFARIKI DUNIA.. HABARI ZIMEINGIA SASA HIVI (kupitia GLOBU YA JAMII) ZINASEMA ABDULHAKIM MAGOMELO MAARUFU KAMA DJ YOUNG KIM(kwenye picha Juu Kushoto Kabisa Enzi za Uhai Wake) HATUNAYE TENA. KWA MUJIBU WA SHEMEJI YAKE, MUDDY BAWAZIR, DJ YOUNG KIM AMEFARIKI KIASI CHA MASAA MAWILI YALIYOPITA AKIWA KATIKA MATIBABU KWENYE HOSPITALI MOJA YA BINAFSI INAYOSHUGHULIKA NA MAGONJWA YA MOYO MAENEO YA MANZESE JIJINI DAR ES SALAAM. DJ YOUNG KIM ATAKUMBUKWA KAMA MMOJA WA MA DJ WAKONGWE WALIOASISI MAMBO KADHAA NCHINI IKIWA NI PAMOJA NA KUPIGA DISKO TOTO (RUNGWE OCEANIC NA BAADAYE MOONDUST DISCO) MASHINDANO YA KWANZA YA KUCHEZA DISKO (YALIYOWATOA KINA BLACK MOSES NA OMMY SYDNEY)PAMOJA NA YO RAP BONANZA(ILIYOMTOA RAPA BORA WA KWANZA WA KISWAHILI SALEH JABIR). GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFUATILIA HABARI HIZI ZA KUSTUSHA NA KUTOA TAARIFA ZAIDI KILA ZINAPOPATIKANA. Mwandishi: haki Tarehe: Tuesday, December 15, 2009 | kiungo mahususi
Sherehe za Elimu Bila Malipo Zafana Pemba.. Mwandishi: haki Tarehe: Tuesday, December 15, 2009 | kiungo mahususi
Nchini Mikono Mitupu.. Kocha wa timu ya Taifa ya Taifa Stars na Kilimanjaro Stars Mbrazili Marcio Maximo Akiongea na Waandishi wa Habari kwenye uwanje wa Ndege wa kimataifa jijini Dar es Salaam jana Muda mfupi baada ya kurudi kutoka nchini kenye kwenye mashindano ya Ccafa Senior Challenge Cup ambapo Tanzania tulitolewa na Kurudi jana Nchini Mikono Mitupu. Picha na Mdau Yusuf Badi |
|
|
|
|
|
|
|